Saturday, January 30, 2016

JENERALI MWAMUNYANGE ABAKISHWA JESHINI HADI 2017, AMIRI JESHI MKUU RAIS MAGUFULI AMUONGEZEA MUDA


Jenerali Mwamunyange, (kulia), akiwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais John Pombe Magufuli, wakati wa kufunga maonyesho ya medani jirani na kambi ya mafunzo ya kijeshi Monduli hivi karibuni.

NA K-VIS MEDIA/
Khalfan Said
MKUU wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, amesema Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amembakiza kuendelea kulitumikia Jeshi hadi Januari 30, 2017.

Jenerali Davis Mwamunyange alikuwa astaafu kazi kesho, Januari 30, 2016, baada ya kulitumikia jeshi hadi kufikia ngazi hiyi ya Mkuu wa Majeshi.
Jenerali Mwamunyange aliwaambia waandishi wa habari makao makuu ya jeshi, Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam kuwa. “Sisi wanajeshi huwa tunabakishwa, Mh. Rais akiona anakuhitaji kumsadia, basi muda wako wa kustaafu ukifika, wewe unabakishwa na anaweza kukuongezea cheo, lakini mimi siwezi tena kuongezewa cheo maana hapa ndio mwisho.” Alisema Jenerali Mwamunyange.
Tayari Mnadhimu Mkuu mpya wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Salvatori Mabeyo, ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama na Utambuzi ya JWTZ, ameapishwa kushika wadhifa huo mpya baada ya mtangulizi wake, Luteni Jenerali Samwel Ndomba, kustaafu.
Majenerali kadhaa wametaafu na tayari wengine wameteuliwa kushika nafasi zao.

0 comments:

Post a Comment